Joshua 19:26-28

26 aAlameleki, Amadi na Mishali. Upande wa magharibi mpaka uligusa Karmeli na Shihor-Libnathi.
27 bTena ukageuka mashariki kuelekea Beth-Dagoni, ukagusa Zabuloni na Bonde la Ifta-Eli, ukaenda upande wa kaskazini hadi Beth-Emeki na Neyeli, ukipitia Kabul upande wa kushoto.
28 cUkaendelea hadi Abdoni, Rehobu, Hamoni na Kana, na kufika Sidoni Kuu.
Copyright information for SwhKC